Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), leo Agosti, 11 limetoa orodha ya timu zinaoongoza kwa ubora duniani na nchi ya Argentina ikiendelea kusalia kileleni ikiwa na alama 1585.

Nafasi ya pili inashikwa na Ubelgiji, nafasi ya tatu Colombia, nafasi ya nne Ujerumani na nafasi ya tano ikishikiliwa na Chile.

Kwa upande wa Tanzania imeshuka kwa nafasi moja kutoka nafasi ya 123 hadi nafasi ya 124 na kwa Afrika Mashariki ikishika nafasi ya 5, nyuma ya Uganda, Kenya, Rwanda na Burundi.

Aidha viwango hivyo vimeonyesha kuwa kwa Afrika, Algeria inaongoza ikifuatiwa na Ghana, Ivory Coast na Senegal ikishika nafasi ya nne.

Mussa Mgosi Aamua Kuwaachia Vijana, Apandishwa Cheo Simba SC
Simba SC Watoa Ufafanuzi Kuhusu Usajili Wa Mavugo