Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA  limeamuru mchezo uliopigwa tarehe 12 mwezi Novemba kati ya timu ya Taifa ya Afrika Kusini na Senegal kurudiwa.

FIFA imetoa uamuzi huo baada ya kamati ya nidhamu ya FIFA kuthibitsha kuwa mwamuzi Joseph Lamptey aliyechezesha mchezo huo hakufanya maamuzi sahihi. Fifa imemfungia maisha mwamuzi Joseph Lamptey kutojihusisha na soka.

Mwamuzi Joseph Lamptey kutoka Ghana aliwapa penati South Africa kimakosa katika kipindi cha kwanza huku timu zote zikiwa 0-0. Mwamuzi huyo alitoa penati akidhani beki wa Senegal Kalidou Koulibaly ameunawa mpira katika eneo la hatari (18 Yard).

Baada ya kupitia picha za video imegundulika kuwa mpira uligonga katika goti la beki wa Senegal Kalidou Koulibaly na sio katika mkono wake.

Katika mchezo huo yalitokea maamuzi mengi yakutatanisha

Katika mchezo huo timu ya South frica maarufu kama Bafana Bafana iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Simba wa Teranga ‘Senegal’.

Mchezo huo utarudiwa mwezi Novemba mwaka 2017 katika kalenda ya kimataifa ya FIFA kwenye tarehe ambayo itatajwa.

 

 

Video: Ndugai atoa ufafanuzi kuhusu matibabu ya Lissu
Tutawashangaza watu, goli saba si kitu kwetu- Masau Bwire