Shirikisho la Mpira wa Magongo Duniani (FIH) limeandaa mashindano ya mchezo huo yatakayofanyika mwezi Februari mwaka 2017 mkoani Arusha.

Rais wa FIH, Leandro Negre amesema shirikisho hilo litahakikisha mpira wa magongo nchini unarudi katika kiwango chake cha awali na kwamba lina andaa michuano mbalimbali ya kitaifa na kimataifa ili kuurejesha mchezo wa mpira wa magongo.

Rais wa Mpira wa Magongo nchini Abraham Sykes amesema miaka ya 1980 Tanzania ilikuwa inafanya vizuri katika michuano hiyo ambapo mwaka 1980 ilishinda kombe la dunia la mchezo huo.

Amesema kilichofanya mchezo huo ushuke kiwango hapa nchini ni kuwa wachezaji waliokuwa na uzoefu wa mchezo huo walihama nchini.

Pia amesema mara ya mwisho Tanzania kushiriki michuano ya mpira huo ilikuwa mwaka 1987 na kwamba haijashiriki kwa kipindi kirefu na kupelekea mchezo huo kisahaulika nchini.

Audio: Kamanda Msangi atoa taarifa ya ajali ya Basi la Super Shemi
Drfa Yazipongeza Kilimanjaro Queens Na Serengeti Boys