Filamu mpya ya Star Wars: The Force Awakens ambayo ndani yake yumo muigizaji wa kike raia wa Kenya, Lupita Nyong’o  imevunja rekodi za mauzo ya filamu duniani baada ya kuingiza zaidi ya dola bilioni 1.2 ($1.2 billion) ndani ya siku 12 tu.

Star Wars: Force Awakens iliyotoka hivi karibuni iliingiza kiasi kikubwa cha fedha kupitia majumba mbalimbali ya sinema katika kipindi cha sherehe za Christmas.

Filamu hiyo iliyoongozwa na JJ Abrahams imeifunika filamu ya Jurassic World iliyoingiza kiasi hicho cha fedha ndani ya siku 13 mwezi Juni ikiwa ni pamoja na kiasi ilichokusanya kwa kuoeneshwa nchini China, huku The Star Wars mpya ikiingiza kiasi hicho kabla haijaanza kuoneshwa nchini China.

The Force Awakens ilianza kuoneshwa kwa mara ya kwanza Los Angeles Desemba 14. Ni filamu ya saba katika mfululizo wa filamu za The Star Wars.

Mke wa T.B Joshua aeleza jinsi alivyoanza Mapenzi na Mumewe, Aulizwa alivyo 'Kitandani'!
Dar24 Kuzindua App Mpya ya Simu Za Android, Ni zawadi Bora ya Mwaka 2015/16