Nchi ya Finland imeipongeza Tanzania kwa hatua mpya za kimaendeleo katika nyanja za ushirikishwaji wa sekta binafsi, uhuru wa vyombo vya habari,utawala bora na haki za binadamu pamoja na mapambano dhidi ya UVIKO 19.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Liberata Mulamula amesema Tanzania na Finland zimekuwa na ushirikiano wa muda mrefu tangu Tanzania ilipopata Uhuru ambapo Finland imekuwa ikisaidia kukuza na kuendeleza sekta za kimaendeleo hususan Elimu, Afya, Utalii, Mazingira pamoja na Maliasili.

“Katika jitihada za kuendeleza ushirikiano wetu na Finland,imeandaa mpango mkakati wa maendeleo katika nyanja mbalimbali kama vile masuala ya misitu, utawala bora, haki za binadamu na masuala ya kuendeleza wanawake ambapo nimepokea rasimu ya mpango huo leo na nitaufanyia kazi ili tuweze kuendeleza ushirikiano wetu kwa maslahi ya mataifa yetu,” Amesema Balozi Mulamula.

Balozi wa Finland hapa nchini Riitta Swan ametoa pongezi hizo wakati alipokutana kwa mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam.

Balozi Mulamula, Balozi Riitta Swan wamekutana kwa lengo la kuwasilisha mpango mkakati wa miaka minne wa Finland katika nyanja za mashirikiano na Mataifa mengine ikiwemo kukuza na kuendeleza diplomasia ya uchumi kupitia biashara na uwekezaji.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula akimkaribisha Balozi wa Finland hapa nchini Mhe. Riitta Swan wakati walipokutana kwa mazungumzo katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) wakati wa mazungumzo baina yao yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula (Mb) akiteta jambo jambo na Balozi wa Finland nchini Mhe. Riitta Swan wakati wa mazungumzo yaliyofanyika katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam
Maongezi baina ya Balozi wa Finland Riitta Swan na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula yakiendelea katika Ofisi Ndogo za Wizara Jijini Dar es Salaam



Kiongozi wa mpito Mali anusurika kuchomwa kisu
Serikali kudhibiti ongezeko bei ya mbolea