Wawindaji wa Mwanza wilayani Misungwi kutoka vijiji vya Sumbugu na Ilujamate wamewaua fisi 12 siku chache mara baada ya mtoto wa miaka 6 kuliwa na kuuawa na fisi hao.

Martha ambaye ni mwanafunzi wa darasa la pili aliualiwa na fisi mnamo Aprili 25 mwaka huu alipokwenda kujisaidia baada ya kumaliza chakula cha usiku.

Baada ya tukio hilo kamati ya ulinzi na usalama ya vijiji hivyo chini ya Mwenyekiti wao, Samweli Welesi walikubaliana kutafuta wawindaji wa jadi wenye ujuzi wa kuwaua wanyama hao na kuamuru kila kaya kuchangia sh 1500 ili kufanikisha kazi hiyo.

Kiongozi wa wawindaji hao, Ngubila Mnigwa amesema walifika kijijini hapo juzi wakiwa 80 na mbwa 90, walifanikiwa kuwaua fisi 10 huku mmoja akikutwa na shanga kiunoni na kuwanasa watoto wawili wa wanyama hao.

Aidha amesema msako unaendelea na watahakikisha wanawasambaratisha wote ili kurejesha kwa amani kwenye kijiji.

Taarifa rasmi kuachiwa kwa Lulu Michael Rais Magufuli ahusika
Man United yawapiku Man City, Barca, Madrid