Mshambuliaji wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans Fiston Kalala Mayele amempongeza Mshambuliaji wa Geita Gold FC George Mpole kwa kufanikiwa kuwa Mfungaji Bora msimu wa 2021/22.

Mpole alimaliza msimu jana Jumatano (Juni 29) kwa kufunga bao lake la 17 wakati wa mchezo dhidi ya Coastal Union, iliyokua nyumbani CCM Mkwakwani jijini Tanga.

Mayele ametuma pongezi kwa Mpole kwa kuandika ujumbe katika ukurasa wake wa Instagram, hatua ambayo imeonyesha amekubali kushindwa katika mbio hizo za ufungaji Bora.

Mayele ameandika: @officiall_georgempole Nichukue nafasi hii kutoka ndani ya moyo wangu kukupongeza Kwa jitihada zako kufanikiwa kuwa mfungaji bora Kwa kufunga mabao 17 katika msimu wa 2021/2022 nakutakia kila la kheri.

Wakati Mpole akimaliza msimu wa 2021/22 kwa kufikisha mabao 17 (Penati Mbili), Mayele amebaki nafasi ya pili kwa kuwa na mabao 16 (Penati Moja).

Polisi wajeruhiwa wakiwatawanya waandamanaji
Habari kuu kwenye magazeti ya leo Juni 30, 2022