Mwanamitindo maarufu kutoka nchini Tanzania, Flaviana Matata ametokea kwenye tangazo la bidhaa mpya za urembo za mwimbaji Rihanna fenty ‘Beauty’.

Rihanna amekuwa akiwatumia wanamitindo tofauti tofauti katika matangazo ya bidhaa zake za urembo hasa wanamitindo wa Kiafrika akiwemo Slick Wood pamoja na flaviana Matata ambaye ameonekana katika tangazo hilo baada ya mwanamziki huyo kuweka picha kwenye ukurasa wake wa instagram.

Aidha bidhaa hizo zinatajwa kuwa ziko sokoni tayari tokea Machi 21,2019.

Nakushukuru wewe pamoja na timu yako kwa kuniruhusu kuwa mmoja wa hii, najivunia kwa kila kazi ambayo mnafanya lakini cha muhimu zaidi ni kuwawakilisha wanawake wote, napenda kile ambacho bidhaa zenu zinasimamia,”amesema mwanamitindo Flaviana Matata.

 

 

Jamani Ikulu isikieni tu, kitete kilinijaa- Manara
Sababu vifo vya ghafla yatajwa

Comments

comments