Hatimaye Kocha Mkuu wa RS Berkane ya nchini Morocco, Florent Ibenge, ametaja sababu za kushindwa kumtumia Kiungo Mshambuliaji kutoka nchini Zambia Clatous Chama.

Chama ambaye kwa sasa amekua gumzo nchini Tanzania akihusishwa na mpango wa kujiunga na moja ya timu za Kariakoo (Simba SC na Young Africans), amekua na wakati mgumu wa kupata nafasi ya kudumu kwenye kikosi cha kwanza cha RS Berkane.

Kiungo huyo asajiliwa na RS Berkane mwanzo wa msimu huu akitokea kwa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC sambamba na Winga kutoka DR Congo Tuisila Kisinda ambaye aliyekua akiitumikia Young Africans.

Kocha Ibenge amesema suala la Chama kutokupata nafasi ya kucheza mara kwa mara ndani ya kikosi chake inatokana na mchezaji huyo kushindwa kuendana haraka na mazingira ya timu, jambo ambalo linahitaji muda kidogo kwa mchezaji huyo kukaa sawa.

“Chama kushindwa kupata nafasi ya kucheza mara kwa mara inatokea kwa wachezaji wengi wakubwa duniani ambao baada ya kuhama kutoka sehemu moja kwenda nyingine wanashindwa kuendana na mazingira ya timu haraka, jambo ambalo baadae hubadilika baada ya kuyazoea mazingira, ni kama tu ilivyotokea kwa Chama.

“Hivyo Chama anahitaji muda wa kuyazoea mazingira ya timu ambayo ni mpya kwake, naamini atakuja kukaa sawa, Chama ni mchezaji mzuri mwenye uwezo mkubwa wa kucheza timu yoyote barani Afrika, hivyo ndio maana hata sisi tulimsajili, naamini kila kitu kitakuwa sawa huko mbeleni, ni jambo la muda tu.” amesema kocha huyo ambaye aliahi kukinoa kikosi cha timu ya taifa ya DR Congo.

Wakuu wa Mikoa wapigwa misasa anuani za makazi
86% ya Watanzania wanakosa matibabu kwa kukosa Bima