Rais wa klabu ya Real Madrid Florentino Perez hayupo kwenye hali nzuri na kiti chake kwa sababu mashabiki wanaonyesha wazi kwamba hawamtaki tena aongoze club hiyo.

Mara nyingi uwanjani kuna mabango yanaonyesha hisia zao kwamba hawamtaki tena aongoze club yao. Gazeti la El Confidencial limetoa ripoti za ndani kwamba Rais huyo ana mpango wakukataza mabango yote ambayo yanatoa ujumbe negative ndani ya uwanja wa Bernabeu.

Moja kati ya mabango ambayo yalionekana kwenye uwanja wa Bernabeu yalikua yanasema hivi, “Listen to the Stadium and Step Down”. Bango hilo baada ya muda lilitolewa na gazeti hilo la El Confidential linasema lilikua ni agizo la Perez kwenda kwa security wa uwanja.

1

Habari mbaya zaidi kwa Real Madrid kutoka kwa gazeti hilo ni kwamba licha ya Ronaldo kuendelea kucheza vizuri binafsi na kutupia magoli, bado mpango wake wa kusepa kwenye club hiyo anao japokua binafsi anazungumzia na kuonekana kwamba atacheza hapo kwa miaka mingi zaidi.

Utaupenda waraka huu kwa Rais Magufuli kuhusu Utumbuaji Majipu
Kocha Wa Coastal Union Ampongeza Muamuzi Kwa Kupoteza Point Tatu Ugenini