Florentino Pérez Rodríguez, ataendelea kuwa rais wa klabu bingwa nchini Hispania na barani Ulaya (Real Madrid), hadi mwaka 2021.

Taarifa iliyotolewa na klabu hiyo ya mjini Madrid imeeleza kuwa, maamuzi hayo yamefikiwa baada ya wadau wa Real Madrid kushindwa kujitokeza kwenye mchakato wa kufanya uchaguzi katika nafasi ya urais.

Jana jumapili ilikua mwisho kwa wadau wa soka wa klabu hiyo kujitokeza hadharani na kuthibitisha kama watawania kiti cha urais, hali ambayo inaendelea kumpa nafasi Parez ya kuwa rais kwa kipindi kingine cha miaka minne ijayo.

Perez, alirudi maradakani mwaka 2009 na amekua mpambanaji kwa kila hali, hadi kufikia mafanikio ya kutwaa ubingwa wa Ulaya mara tatu ndani ya miaka minne iliyopita.

Katika utawala wa miaka minane iliyopita, kiongozi huyo pia ameiwezesha Real Madrid kutwaa ubingwa wa Hispania (La Liga) mara mbili.

Mipango ya usajili, na kuwa na benchi bora la ufundi, imekua nyenzo kwa kiongozi huyo kuunda kikosi chenye ushindani wakati wote tangu aliporejea maradakani kwa mara ya pili.

Perez aliiongoza Real Madrid kwa mara ya kwanza kama rais mwaka 1995, na aliendelea hadi mwaka 2002.

Ureno yatangaza siku tatu za maombolezo
Cameroon yashindwa kutamba mbele ya Chile

Comments

comments