Mmarekani mweusi mwenye umri wa miaka 46, George Floyd, anazikwa leo mjini Houston, ambako alikulia kando ya kaburi la mamake katika hafla ya faragha.

Wakati hayo yakijiri, Derek Chauvin, polisi wa zamani ambaye ni mshukiwa mkuu katika mauaji , amewekewa dhamana ya dola milioni moja.

Jaji anayeendesha kesi hiyo alitangaza masharti kadhaa ya kuwachiwa kwake kwa dhamana. Mshukiwa huyo hapaswi kuondoka jimbo la Minnesota baada ya kuwachiwa, asiwasiliane na familia ya Floyd na lazima asalimishe silaha zote anazomiliki.

Aidha haruhusiwi kufanya kazi katika nafasi yoyote kwenye idara ya usalama. Polisi wengine watatu wa Minneapolis walifikishwa mahakamani wiki iliyopita wakikabiliwa na mashitaka ya kusaidia katika mauaji ya Floyd. Wote wanne wamefutwa kazi.

Mapema leo, maelfu ya watu walijitokeza kutoa heshima zao mjini Houston jimbo la Texas. Jeneza lake lililokuwa wazi lilipelekwa katika kanisa la The Fountain of Praise ambapo karibu watu 6,000 walifika kumuaga.

Kifo cha Floyd kimebadilisha picha ya ulimwengu na kuamsha upya mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi na ukatili wa polisi.

Mchungaji Mashimo ahusishwa uvamizi wa Mbowe
Chanjo ya Ebora imeanza kutolewa COngo