Mwanamuziki maarufu nchini Nasibu Abdul maarufu ‘Diamond Platnumz’ anayetamba na albamu ya First of All (FAO) amefanikiwa kushinda tuzo ya album bora kwa mwaka 2022 kwenye tuzo za kimataifa za African Entertainment Awards (AEAUSA) zilizotolewa usiku wa kuamikia leo januari 1, 2023 huko nchini Marekani.

Taarifa za ushindi wa tuzo hiyo zimemfikia Diamond akiwa katika onyesho lake la funga mwaka (Cheers 2023) liliyofanyika usiku wa Desemba 31, 2022, Ramada hotel jijini Dar es salam.

First Of All EP, iliachiwa rasmi Machi 12, 2022 ikiwa na jumla ya nyimbo kumi, ambazo ndani yake ni takribani nyimbo nne pekee ndio alizoshirkiana na wasanii wengine akiwamo Adekunle Gold kutoka Nigeria, Mbosso, Zuchu pamoja na Jaywillz.

Also read: Diamond afichua siri za Marioo kumuomba ya WCB

Tuzo za AEAUSA kwa mwaka 2022, ni tuzo za nane kutolewa tangu kuanzishwa kwake ambapo ‘FOA’ ilifanikiwa kuingia kwenye kinyang’anyiro cha album bora za mwaka ikiwa katika ushindani mkali na album nyingine kama ‘Catch me if you can’ ya Adekunle Gold, ‘The Guy’ ya Mi Abaga, ‘Rave & Roses’ ya Rema pamoja na ‘Affection’ ya Magasco Bboy.

Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Januari 2, 2023
Gari lapinduka sokoni, 10 wafariki