Watu 15 wameripotiwa kufa wakiwa katika foleni kubwa ya magari katika makutano maarufu ya barabara ijukanayo kama Brexit jijini Java nchini Indonesia. Foleni iliyodumu kwa takribani siku 3.

Wizara ya afya nchini humo imethibitisha kutokea kwa vifo hivyo wakati watu wakielekea kusherehekea sikukuu ya Eid El- Fitr. Imesema msongamano huo mkubwa wa magari ulisababisha kuongezeka kwa joto kwa kiasi kikubwa katika eneo hilo na kukosekana kwa hewa safi kutokana na moshi mwingi wa magari.

Udah teler nihh yah… Kena maceeettt ?????bucukkk kita.. Panassss ???

A photo posted by Megga (@megga_wee) on

Wizara hiyo ya afya ilieleza kuwa watu wengi walifariki kutokana na kukaukiwa maji, kukosa hewa ya kutosha pamoja na magonjwa ya moyo. Walioathirika zaidi ni kundi la watoto na wazee.

Chanzo cha msongamano huo wa magari uliofikia urefu wa kilometa 20 ni wimbi la watu waliokuwa wakiondoka mijini kuelekea vijijini kwao kusherehekea sikukuu ya Eid, Jumatano wiki hii.

Msemaji wa wizara ya uchukuzi, Hemi Pramuraharjo ameiambia AFP kuwa familia zilikwamba kwenye magari binafsi na mabasi na joto kali kwa siku tatu. Alisema vifo vilitokea kati ya July 3 hadi 5.

TCRA yailima adhabu Clouds TV kwa kurusha kipindi cha Ushoga
Polisi Watano wauawa katika maandamano ya kupinga mauaji ya Weusi Marekani