Mfumo wa kiteknolojia wa AdaLipa ambao upo chini ya kampuni ya DataVision International umefanikiwa kupunguza muda unaotumiwa na wazazi kuwalipia ada watoto wao mashuleni. AdaLipa imeweza kufanikisha zoezi zima la ulipaji wa ada moja kwa moja kwa kutumia simu zao za mkononi.
AdaLipa inafanya kazi na mashule ya Tanzania kuyawezesha kurahisisha ukusamyaji na ulipaji ada chini ya dakika tano. Mashule yaliyojiunga na AdaLipa yamefanikiwa kuweza kupata taarifa za papo kwa papo juu ya utendaji katika zoezi zima la malipo ya ada na kurahisisha malipo kwa upande wa wazazi.
Mmoja wa wakilishi wa AdaLipa, MacLean Geofrey aliongezea pale alipoulizwa Teknolojia hii ina faida gani katika wigo mzima wa elimu, alijibu, “Maisha ya mtanzania wa kawaida yanabadilika kwa kasi sana. Kadri miaka inavyoenda watanzania wengi zaidi wamekuwa wakimiliki simu za mkononi na hivyo kuwapa wabunifu njia nyingi zaidi za kutumia simu. AdaLipa ni mfumo rahisi unaokuwezesha kuepuka adha za malipo ya ada kama muda, foleni na kadhalika”
Kwa kujua zaidi kuhusu mfumo huu, wapigie simu 0715222132 au email info@mlipa.co.tz