Huku Taifa la kenya likisubiri Mwenyekiti wa Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) Wafula Chebukati kutangaza matokeo ya urais wakenya wamekuwa wakijaribu kufahamu kuhusu fomu 34A ambazo zimechukua nafasi kubwa katika shughuli ya kujumuisha kura.

Kulingana na (IEBC) kuna aina tofauti zinazotumiwa katika mchakato wa uthibitishaji wa matokeo ya uchaguzi wa urais.

Orodha za fomu zinazotumika kuhesabu kura katika Uchaguzi Mkuu Kenya ni 34A, 34B, 34C.

Fomu 34A inatumika kuandika matokeo kutoka katika vituo vya kupigia kura, karatasi hii inajazwa na kutiwa saini na wasimamizi wa Uchaguzi wa Kaunti na kisha kuwasilishwa kwa Tovuti ya IEBC na kufikishwa katika kituo cha kitaifa cha kupigia kura.

Fomu hiyo inajumuisha kura ambazo kila mgombea urais alipata jumla ya idadi ya wapiga kura waliojiandikisha katika kituo hicho.

Fomu 34B, hati hiyo inatumiwa kukusanya nambari zote kutoka vituo tofauti vya kupigia kura na kuziweka chini ya mabano ya ngazi ya eneo bunge.

Inajumuisha misimbo ya vituo vya kupigia kura, jina la kituo nambari ya wapiga kura waliojiandikisha jumla ya kula kwa kila mgombea na idadi ya kura halali zilizopigwa.

Hii ina maana kwamba kuna fomu 290 34B zinazowakilisha idadi ya maeneo bunge, mchakato huu husaidia kudhibitisha kama kile kilichoonyeshwa katika fomu 34A kinalingana na kilichopo katika fomu 34B.

Fomu 34C huu ni mkusanyiko wa fomu zote 34B kuwa hati moja, ni waraka rasmi ambapo mwenyekiti Chebukati atatangaza matokeo na kumtangaza Rais.

Mchakato wa udhibitishaji hati huchukua muda kwani fomu moja inaweza kujazwa na afisa mmoja mahali popote kati ya dakika 20 hadi 30.

UN yasikitishwa na mauaji ya Watoto Gaza
Sure Boy: Tumejiandaa kutwaa Ngao ya Jamii