Jarida la Forbes limetoa orodha ya wanamuziki wa Hip Hop ambao wamefanikiwa kuingiza kiasi kikubwa zaidi cha fedha ndani ya kipindi cha mwaka mmoja (Hip Hop Cash Kings), ikimuweka Jay Z kileleni akiwa na $76.5 milioni .

Kwa mujibu wa orodha hiyo ambayo inahusu kiasi cha fedha kilichoingizwa kati ya Juni 2017 na Juni 2018, ni  kiasi chote bila kupunguza matumizi ya kuwalipa mameneja wa wasanii na kabla ya kukatwa kodi.

Diddy ameendelea kuwa karibu na kilele, akimfuatia Jay Z kwa $64 milioni.

Aliyewashtua wengi ni rapa Kendrick Lamar ambaye hakutarajiwa sana mwaka huu, lakini ameonekana kufanikiwa kuingiza $58 milioni, akimpita Drake $47 milioni.

Hii ni orodha kamili ya nafasi 20 za juu:

  1. JAY-Z $76.5 milioni
  2. Diddy $64 milioni
  3. Kendrick Lamar $58 milioni
  4. Drake $47 milioni
  5. J. Cole $35.5 milioni
  6. Dre $35 milioni
  7. Nas $35 milioni
  8. Pitbull $32 milioni
  9. Future $30 milioni
  10. Kanye West $27.5 milioni
  11. DJ Khaled $27 milioni
  12. Migos $24.5 milioni
  13. Eminem $23 milioni
  14. Chance The Rapper $21.5 milioni
  15. Travis Scott $21 milioni
  16. Birdman $20 milioni
  17. Lil Uzi Vert $19.5 milioni
  18. Lil Wayne $19 milioni
  19. Logic $17 milioni
  20. Swizz Beatz $15 milioni
  21. Meek Mill $15 milioni
  22. Russ $15 milioni

Hata hivyo, kwa taarifa yako; ukiachana na orodha hii ya wasanii wa hip hop na RnB, hivi karibuni Forbes ilieleza kuwa Kylie Jenner ndiye msanii mwenye umri mdogo (miaka 21) aliyeingiza kiasi kikubwa ndani ya kipindi cha mwaka mmoja.

Kylie alitajwa kuwa ametengeneza $166.5 milioni ambazo ni mara mbili ya Jay Z.

Mrembo huyu wa familia ya Kardashians anaripotikuwa kuwa na utajiri wa $900 milioni, hivyo ni bilionea mtarajiwa wa kwanza mwenye umri mdogo.

Kylie na utajiri mkubwa kuliko dada yake Kim Kardashian. Lakini sio tu utajiri wa kifedha, anashikilia nafasi ya nane kwa kuwa mtumiaji wa Instagram mwenye wafuasi wengi zaidi, akiwa na wafuasi zaidi ya milioni 114 akitumia @kyliejenner.

Watendaji wa Serikali wapigwa marufuku kusimamia uchaguzi
McGregor matatani tena kwa kumpasua usoni mpiganaji