Jarida la Forbes limetangaza orodha mpya ya majina matano ya wasanii wa Hip Hop wenye ukwasi mkubwa zaidi duniani kwa mwaka huu.

Kama ilivyokuwa kwa mwaka jana, Diddy ameendelea kuiongoza orodha hiyo akiwa na utajiri wa wa dola milioni 750.

Diddy

Diddy

Rapa Drake ameingia kwenye orodha hiyo akimpiga kikumbe 50 Cent ambaye alikuwa katika orodha hiyo mwaka jana. Drake ametajwa kuwa na kipato cha dola milioni 60 zilizotokana na matamasha aliyoyafanya na nakala ya kazi zake alizouza pamoja na dili za matangazo na ubalozi  wa bidhaa na huduma.

Hii ndio orodha kamili:

  1. Diddy ($750 million)
  2. Dr. Dre ($710 million)
  3. Jay Z ($610 million)
  4. Birdman ($110 million)
  5. Drake ($60 million)
Picha: Daladala yaacha njia na kugonga basi la mwendo kasi
Tanzia: Rais wa Zamani wa Burundi afariki