Mtendaji mkuu wa klabu ya Malaga CF ya nchini Hispania Francesc Arnau amesema waliweka dhamira ya kutaka kumsajili mshambuliaji Mario Balotelli wakati wa majira ya kiangazi.

Arnau amesema walikua katika mpango huo kutokana na kuamini huenda mshambuliaji huyo angeweza kuleta changamoto katika safu yao ya ushambuliaji, lakini walikwama katika suala la malipo yake ya mshahara wa kila mwishoni mwa juma.

Amesema Balotelli alihitaji kiasi kikubwa cha pesa ambacho walishindwa kuthibitisha kulimpa, hivyo mpango wa wa kumsajili ulizimika rasmi, na siku chache baadae walisikia amejiunga na klabu ya Nice ya nchini Ufaransa.

“Tulishindwa katika suala la kulipa mshahara wake wa juma, kilikua kiasi kikubwa sana cha pesa ambacho tulikitathmini na kuona tusingeweza kumlipa,” alisema Arnau alipohojiwa na Cadena Cope.

“Alikwenda Nice, kwa sababu wenzetu walikua na uwezo mkubwa kifedha na kwa sasa wanamlipa mshahara ambao kwetu ulikua mtihani kuufanikisha.”

Video: Majaliwa afanya ukaguzi ujenzi wa Magomeni Kota, Ataka ukamilishwe kwa wakati
Kumekucha Azam Sports Federation Cup