Hatimae uongozi wa Swansea City umetangaza kumfuta kazi meneja kutoka nchini Italia Francesco Guidolin baada ya kuchoshwa na mwenendo wake wa kazi.

Swansea City wamechukua maamuzi hayo huku wakimtangaza aliyewahi kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Marekani Bob Bradley kuwa mkuu wa benchi la ufundi klabuni hapo.

Guidolin amekua na wakati mgumu tangu kuanza kwa msimu huu wa ligi na mpaka hii leo anaonyeshwa mlango wa kutokea alikua ameshapoteza michezo mitano ya ligi kuu ya England na mmoja wa kombe la ligi (EFL Cup).

Bradley anakwenda Liberty Stadium akitokea nchini Ufaransa alipokua akikinoa kikosi cha klabu ya Le Havre inayoshiriki ligi daraja la pili.

Video: Polisi Dar kuwakamata waliofanya vurugu mechi ya Simba na Yanga
Video: "Prof. Lipumba kawekwa na ccm" - Mtatiro