Klabu ya Kagera Sugar inahusishwa na mpango wa kumuajiri Kocha Mkuu wa Biashara United Mara Francis Baraza, ili kurithi mikoba iliyoachwa na kocha mzawa Mecky Mexime.

Kagera Sugar wanatajwa kuwa kwenye mpango huo, baada ya kuridhishwa na kazi ya kocha huyo kutoka nchini Kenya, ambaye ameifikisha Biashara United Mara katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara msimu huu 2020/21.

Taarifa zinadai kuwa Kocha Baraza tayari ameshaanza mazungumzo na uongozi wa klabu hiyo yenye maskani yake makuu mkoani Kagera, na kama mambo yatakwenda vizuri huenda akatangazwa wakati wowote kuanzia sasa.

Kocha Mecky Maxime alichimbishwa Kagera Sugar mwishoni mwa juma lililopita kufuatia kikosi cha klabu hiyo kuwa na mwenendo  mbovu kwa msimu huu 2020/21.

Mchezo wa mwisho kwa kocha huyo ambaye aliwahi kuwa nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ kukaa kwenye benchi kabla ya kufutwa kazi ilikuwa Uwanja wa Kaitaba ambapo timu yake iliyeyusha pointi tatu kwa kufungwa na Namungo FC.

Baada ya dakika 90 kukamilika ubao wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 0-1 Yanga jambo ambalo liliwafanya mabosi wa Kagera Sugar kuamua kuachana naye jumlajumla.

Matatani kwa kukutwa na kilo 30. 6 za heroine
Kaze arudisha 'KOMBORA' Young Africans