Benchi la ufundi la klabu ya Arsenal limeanza kusaka mbinu mbadala za kuitengeneza safu yake ya ulinzi kuelekea msimu mpya wa ligi ya nchini England, baada ya changamoto zilizojitokeza kwa wachezaji wanaohusiska na nafasi hiyo.

Kuumia kwa beki kutoka nchini Ujerumani Per Mertesacker pamoja na kuchelewa kwa beki Laurent Koscielny ambaye bado yupo kwenye mapumziko baada ya kumaliza majkukumu ya kuitumikia timu yake ya taifa ya Ufaransa kwenye fainali za Euro 2016, kumetoa nafasi kwa Arsene Wenger na wenzake kubuni mbinu mbadala.

Kiungo kutoka nchini Ufaransa Francis Coquelin, ameripotiwa kuwa katika mazoezi maalum ya kuziba nafasi ya ulinzi katika michezo ya kujipima nguvu itakayochezwa katika kipindi hiki cha kujiandaa na msimu mpya wa ligi.

Jack Wilshere ameandika katika mtandao wa Snapchat, kuhusu mpango huo wa Coquelin kunolewa kwa ajili ya kukaa katika safu ya ulinzi.

Coquelin amekua tegemeo kubwa la Arsenal katika nafasi ya kiungo mkabaji kwa misimu miwili iliyopita, na alionyesha kucheza kwa kujiamini wakati wote hadi kufikia hatua ya kumvutia Arsene Wenger ambaye aliwahi kumtoa kwa mkopo kwa vipindi vitatu tofauti.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka alipelekwa kwa mkopo kwenye klabu za Lorient (2010–2011), SC Freiburg (2013–2014) pamoja na Charlton Athletic (2014).

Wakati huo huo kuna matarajio makubwa kwa Arsenal kuwatumia Gabriel Paulista na Calum Chambers kama mabeki wa kati katika mchezo wa ufunguzi wa ligi ya nchini England ambao utawakutanisha na Liverpool.

Calum Chambers ni beki pekee kwa sasa aliye fit katika kikosi cha Arsenal

Alexandre Pato Kucheza Soka Hispania
Justin Bieber apiga chini dili nono la filamu, akataa kuigiza kama ‘Shoga’