Mshambuliaji kutoka nchini Togo Francis Kouassi Koné amefanikiwa kuokoa maisha ya mlinda mlango wa Martin Berkovec, ambaye alikaribia kumeza ulimi wakati wa mchezo wa ligi ya Jamuhuri ya Czech hapo jana.

Mshambuliaji huyo anaeitumikia klabu ya Slovacko, alibeba jukumu la kumpatia huduma ya kwanza Berkovec, baada ya kugongana na mchezaji mwenzake wa Bohemians 1905, Daniel Krch.

Kone alitumia vidole vya mkono wake wa kulia kuurudisha ulimi wa mlinda mlango huyo katika hali yake ya kawaida, kabla ya watu wa huduma ya kwanza hawajaingia uwanjani.

Baadae Berkovec alimshukuru mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook: “Ninapenda kumshukuru Francis Kone kwa kuokoa maisha yangu, daima nitaendelea kuukumbuka na kuuthamini mchango wake mkubwa alioutoa dhidi yangu, ninarudiia tena kwa kumshukuru na kumwambia ahsante sana!!!”

Arsene Wenger Apiga Teke Fuko La Hela
TFF Yaufungulia Uwanja Wa Jamuhuri