Aliyekuwa Kocha Mkuu Simba SC Franco Pablo Martin ameikana Klabu ya Simba SC inayotajwa kumleta nchini kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kuongeza nguvu katika Benchi la Ufundi la Klabu hiyo ya Msimbazi.

Simba SC inaendelea na Mchakato wa Kumsaka Kocha Mkuu Mpya atakayefanya kazi na Kocha Juma Mgunda, ambaye kwa sasa anakaimu nafasi ya Kocha Mkuu, baada ya kuondoka kwa Kocha Zoran Maki tangu mwezi Septemba.

Kocha Pablo ameonekana jijini Dar es salaam tangu mwishoni mwa juma lililopita na jana Jumapili (Novemba 17) alikuwa Azam Complex-Chamazi akifuatilia mchezo wa Ligi Kuu kati ya Azam FC dhidi ya Coastal Union.

Alipoulizwa Kocha huyo kutoka nchini Hispania alisema amekuja nchini kwa mambo yake Binafsi na hana Mwaliko wowote kutoka Simba SC, inayotajwa kuwa kwenye mpango wa kumrudisha kazini.

“Nipo hapa kiwa mambo yangu binfasi, sina mwaliko wowote na Simba SC, siwezi kukwambia naondoka lini.” alisema Kocha Pablo

Simba SC iliachana na Kocha Pablo Machi 31 mwaka huu baada ya kushindwa kuivusha klabu hiyo kwenye hatua ya Nusu Fainali Kombe la Shirikisho Tanzania Bara, akifungwa na Young Africans bao 1-0.

Rage aipongeza Young Africans, agoma kuipa ubingwa
Habari Kuu kwenye magazeti ya leo Novemba 28, 2022