Klabu za Inter Milan na SSC Napoli zote za nchini Italia, zimeingia katika vita ya kuviziana katika usajili wa washambuliaji wa klabu hizo Mauro Icardi pamoja na Lorenzo Insigne.

SSC Napoli tayari wameshaonyesha nia ya kutaka kumsajili Icardi kwa majuma kadhaa hivi sasa, lakini wamepata ushindani mkubwa wa kutaka kuporwa mshambuliaji wao kutoka nchini Italia Insigne.

Meneja mpya wa Inter Milan Frank de Boer ametangaza mipango ya kutaka kumuhamishia Stadio Giuseppe Meazza mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kama chaguo lake la kwanza mara baada ya kukabidhiwa majukumu ya ukuu wa benchi la ufundi baada ya kuondoka kwa Roberto Mancini.

Mauro Icardi

Mipango ya meneja huyo kutoka nchini Uholanzi, imewashangaza wadau wengi wa soka nchini Italia kwa kuona kama anataka kuchokonoa dili la mshambuliaji wake Icardi kuhamia Stadio San Paolo ambalo tayari lilionekana kufifia.

Hofu hiyo imeibuka kutokana na mpango wa usajili wa De Boer huenda ikasababisha suala la kubadilishana kwa washambuliaji hao wawili, wakati tayari ameshaonyesha msimamo wa kutaka kumtumia Icardi kwenye mipango yake ya msimu wa 2016/17.

Lorenzo Insigne

SSC Napoli waliweka dhamira ya kutaka kumsajili mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 23 kama mbadala Gonzalo Higuain aliyetimkia kwa mabingwa wa soka nchini Italia Juventus FC mwishoni mwa mwezi uliopita.

Kwa upande wa Inter Milan wanahitaji kumsajili Insigne kwa kutaka kuiongezea nguvu safu yao ya ushambuliaji ambayo kwa msimu ujao wa ligi, itapaswa kufanya kazi ya ziada ili kutimiza malengo yanayokusudiwa na De Boer.

Waarabu Kuamua Game Ya Super Eagles Vs Taifa Stars
FA Yapanga Ratiba Ya Mzunguuko Wa Pili Wa EFL Cup