Joto la kupoteza ajira kwa meneja wa klabu ya Inter Milan Frank de Boer lilipanda tena mwishoni mwa juma lililopita (Jana Jumapili), baada ya kikosi chake kushindwa kufurukuta katika mchezo wa ligi kuu ya soka nchini Italia (Serie A) kwa kukubali kufungwa bao moja kwa sifuri dhidi ya Sampdoria.

Katikati ya juma lililopita bodi ya wakurugenzi wa klabu ya Inter Milan ilitoa taarifa za kufanya kikao hii leo na moja ya ajenda zitakazozungumzwa ni mustakabali wa kibarua cha meneja huyo kutoka nchini Uholanzi.

Dhumuni kubwa la mkutano wa viongozi wa juu wa Inter Milan kukutana hii leo, linatokana na subra iliyofanywa miongoni mwao ya kuangalia mchezo wa siku ya jumapili kama wangeweza kupata ushindi, lakini mambo yaliwaendea mrama.

Hata hivyo tayari mmiliki wa Inter Milan Erick Thohir, aliwahakikishia waandishi wa habari siku ya jumatano kuwa, bado wana imani kubwa na De Boer, na hawatarajii kumfuta kazi.

Mara baada ya mchezo wa jana dhidi ya Sampdoria, De Boer alizungumza na vyombo vya habari na kueleza matarajio yake baada ya mpambano huo, ambao matokeo yake yanahatarisha kibarua chache.

“Bado nina matarajio makubwa na kikosi changu, na ninatambua tunapita katika kipindi kigumu. Tupo katika kiwango kizuri lakini changamoto za ushindani katika ligi ni kubwa.

“Sikupendezwa na uwezo wa wachezaji waliouonyesha katika kipindi cha kwanza kwenye mchezo wa leo (jana). Hatukucheza vizuri na ninaamini hapo ndipo tulikosea na kuwapa nafasi wapinzani wetu kucheza kwa kujiamini kwa kiasi kikubwa.

Hata hivyo alipouliza kuhusu mustakabali wa kibarua chake alijibu “Mnapaswa kuuliza uongozi wa klabu, mimi ninaendelea kufanya kazi zangu kama kawaida.”

Jose Mourinho Hana Pakutokea, Kamati Yamsubiri Kwa Hamu
Gareth Bale Kudumu Santiago Bernabeu Hadi 2022