Uongozi wa Klabu ya Everton inatajwa kuwa kwenye mpango wa kumfuta kazi meneja wa kikosi chao Frank Lampard wakati wowote kuanzia sasa.

Maamuzi hayo yanatajiwa kufanywa, kufuatia mwenendo mbaya wa kikosi cha Everton, ambacho hakifanyi vizuri katika Michezo ya Ligi Kuu ya England msimu huu 2022/23.

Lampard alianza kazi rasmi klabuni hapo Januari 2022, na aliisaidia klabu hiyo kubaki Ligi Kuu msimu uliopita kwa kuokota alama 15, baada ya kucheza michezo 20.

Kikosi cha Everton hadi sasa kimecheza michezo kumi pasina kupata ushindi katika Michuano yote, huku klabu hiyo ikishika nafasi ya 19, kwenye msimamo wa Ligi kuu ya England.

Tayari Everton imeshaondolewa kwenye Michuano mingine ya England (Kombe la Ligi na Kombe la FA).

Azam FC yafichua alipo Tape Edinho
Hakuna atakayefungwa kwa kukosa Bima ya afya: Ummy