Takriban watu 40 Ujerumani, wamethibitishwa kuambukizwa virusi vya Corona baada ya kuhudhuria ibada kanisani katika mji wa Frankfurt.

Idara ya afya katika mji huo imesema mtu mmoja kati ya hao 40 ndiye yuko hospitalini na wengine sio wagonjwa wa kuwa hospitali.

Wakati huo huo mamlaka katika mji jirani wa Hanau ulio mashariki mwa jiji la Frankfurt imesema watu wapatao 16 kutoka mji huo wameambukizwa na virusi vya Corona baada ya kuhudhuria ibada ya kanisani mjini Frankfurt.

Ili kuzuia maambukizi zaidi, mamlaka ya mji huo wa Hanau imefutilia mbali hafla nyengine iliyopangwa kufanyika leo katika mji huo.

Waziri Mkuu azindua Kigoma ya mawese, kugawa mbegu bure
Ummy atoa majibu ripoti ya uchunguzi maabara ya corona "mashine ina hitilafu"

Comments

comments