Kufuatiwa kifo cha aliyekuwa waziri wa Usalama nchini Kenya, Jenerali mstaafu Joseph NKaissery, Rais Kenyatta amefanya uteuzi na kumteua Waziri wa elimu Dkt Fred Matiang’i kuwa kaimu waziri wa Usalama wa ndani nchini humo.

Rais Uhuru Kenyatta amefanya uteuzi huo baada ya kuongoza mkutano wa dharura wa Baraza la Usalama Taifa.

”Hakutakuwa na pengo lolote kiusalama nchini kutokana na kifo cha jenerali huyo mstaafu” amesema Kenyata.

Aidha Rais Kenyatta amewaomba wakenya kudumisha utulivu na taratibu ziendelee kama kawaida, mabadiliko yeyote yatakayo tokea vyombo vya habari vitaendelea kuwajuza.

”Na maandalizi ya uchaguzi mkuu ambao utafanyika tarehe 8 Agosti, mwezi mmoja kuanzia sasa, yataendelea bila kuvurugika”, Kenyatta amemalizia kwa kusema hivyo.

 

 

Ommy Dimpoz afunguka alipopata kiburi cha kula bata ‘Dubai’ kama bilionea
Waziri wa Usalama Kenya Joseph Nkaissery afariki dunia, Lowassa atoa neno