Takribani masaa 24 kabla ya Yanga kuwavaa TP Mazembe katika mchezo wa hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, meneja wa mabingwa hao wa ligi ya JK Kongo, Fredrick Kitenge amesema hawakuja kushindana na Yanga.

Kitenge ambaye huwezi kumkosa katika pambano lolote la TP Mazembe amesema kuwa licha ya kushiriki katika mashindano ya Kombe la Shirikisho, ametamba kuwa Yanga ni wachanga mno kushindana nao.

Ameongezea kuwa wamekuja kutupia jicho vipaji kama walivyofanya mwaka 2011 na kufanikiwa kumsajili Mbwana Samatta kutokea Simba na baadaye Thomas Ulimwengu aliyekuwa Moro United kwa mkopo.

” Yanga ni wachanga mno kushindana na TP Mazembe. Hatukuja kushindana nao, tumekuja kutupia jicho vipaji kama tulivyofanya miaka ya nyuma na kufanikiwa kumuona Samatta ” Ametamba Kitenge.

TP Mazembe wamekuja na kikosi cha wachezaji 18 tu ambao wameonekana kutukuwa na wasiwasi kabisa na pambano la kesho katika hoteli ya Serena walipofikia.

Yanga iliyoanza vibaya hatua ya makundi kwa kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa MO Bejaia itashuka dimbani kusaka pointi za kwanza na kurudi katika mstari wa kupigania nafasi ya kufuzu nusu fainali.

Chanzo: Soka360

Baada ya script ya 'Chura' kukataliwa, Snura ameipeleka nyingine kukaguliwa
Kipaji Ndumba Kunanii Diamond Platnumz!!