Ndoa ya mshambuliaji wa pembeni wa Tanzania Mrisho Ngassa na uongozi wa klabu ya Free State Stars ya Afrika kusini imevunjika baada ya pande hizo kukubaliana kuvunja mkataba.

Ngassa ambaye aliwahi kuzichezea klabu za Toto Africans, Kagera Sugar ,Young Africans, Azam FC pamoja na Simba zote za ligi kuu ya soka Tanzania bara amedhihirisha kuvunja mkataba wake, baada ya kuanika hadharani uthibitisho wa barua.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa, Ngassa alikuwa amedhamiria kukatisha mkataba wake na Free State Stars tangu mwezi Agosti, na ndipo Meneja mkuu wa klabu hiyo Rants Makoema alipoamua kufanya nae mazungumzo.

barua ya Ngassa

Hata hivyo Ngassa ametoa sababu za kuamua kuachana na Free State Stars, kwa kusema klabu hiyo imekua haina mafanikio kama alivyotarajia, hivyo ameona ni bora aanze utaratibu wa kusaka mahala ambapo patamuwezesha kutimiza malengo yake.

Wakati maamuzi hayo yakifanywa na Mrisho Ngassa, uongozi wa Free State Stars ulikua umeshajipanga kuziba pengo lake, na tayari wamefanikiwa kumnasa mshambuliaji kutoka nchini Uganda Hamis Kiiza ambaye msimu uliopita aliitumikia Simba Sport Club.

Samir Nasri: Ni Maamuzi Yangu, Pep Guardiola Hapaswi Kulaumiwa
Maandamano ya kupinga matokeo ya uchaguzi Gabon yazua mauaji