Klabu ya Fulham imejihakikishia nafasi ya kurudi katika Ligi Kuu ya England (EPL) baada ya beki wao wa kushoto Joe Bryan, kufunnga mabao mawili katika muda wa nyongeza.

Bryan alifunga dakika ya 105 kwa mpira wa kutengwa kutoka umbali wa yadi 35, huku akionekana kama anapiga ndani ya eneo la hatari, lakini aliupiga moja kwa moja langoni na kumshinda mlinda mlango David Raya wa Brentford.

Brentford walilazimika kumaliza miaka 73 ya kusubiri, baada ya kushindwa kwa mara nyingine katika michezo ya mtoano.

Mchezo huo ulianza taratibu lakini kadri muda ulivyozidi kwenda ulikua ya kuvutia kwa kushambuliana, Katikati ya kipindi cha pili Fulham walinusurika kupata kadi nyekundu baada ya mchezaji wao Tom Cairney kumfanyia madhambi Said Benrhama.

“Nimejifunza mengi katika msimu huu. Nina uhakika nitaendelea kujifunza mengi katika kazi yangu kama kocha, lakini msimu huu hatukupata kitu kikubwa zaidi.

Nilisema mara nyingi kuhusu timu na wapi tulipokuwa msimu uliopita. Tulikuwa na majeraha ya wazi ambayo labda mtu mwingine wa nje hawezi kuyaona.” alisema Scott Parker meneja wa Fulham.

Fulham anarejea katika Ligi Kuu ya EPL baada ya kushuka msimu wa 2018/19.

Polepole''CHADEMA waombe radhi kubadili wimbo wa Taifa''
Young Africans wamnasa David Richard