Rais Samia Suluhu Hassan usiku wa kuamkia Leo ameongoza uzinduzi wa makala ya Runinga ya ‘Tanzania:The royal Tour’ uliyofanyika New York Marekani na Kusema

Katika Uzinduzi huo ambao ni kwa awamu ya kwanza huko New York, ni sehemu ya Mikakati mbalimbali anayotekeleza kukuza na kuimarisha uchumi na Ustawi wa Tanzania, ameweka historia kubwa ya kuitangaza Tanzania duniani kote, maliasili za utalii, na fusra nyingine za kibiashara na uwekezaji zilizoko nchini.

Kupitia uzinduzi huo ambayo muhusika mkuu ni Rais Samia Suluhu akiwa amevalia mavazi ya safari za mbugani, watazamaji wa dunia nzima watapata fursa ya kuona kwa kifupi na kwa mbali urithi, mandhari, na taswira ya kipekee ya utajiri wa kihistoria uliopo katika kila kona ya Tanzania.

Watazamaji pia wataona Utajiri wa Tanzania, katika ameneo yote kuanzia Zanzibar, Ngorongoro, Serengeti, Olduvai Gorge, Mlima Kilimanjaro, Mikumi, Hifadhi ya Ruaha, na Pori la akiba la Selous, maeneo maarufu ya Pwani ya Bahari ya Hindi, uvuvi bora katika visiwa vya Mafia na Pemba.

Pia wataona urithi wa utamaduni na Sanaa ambao utajumuisha shughuli na Maisha ya makabila mbalimbali wakiwemo wamasai, wasukuma, wamakonde, na wengine bila kusahau Maisha ya waswahili katika pwani ya bahari ya hindi.

Lengo kuu kupitia mkakati huu ni kutengeneza fursa za ajira, kuongeza watalii, kuongeza kipato cha mtu mmoja mmoja, kuongeza pato la taifa, na kuweka mazingira ya kukuza uchumi wa mtu, kundi na taifa kwa ujumla.

Filamu hiyo ya Tanzania:The Royal Tour ilirekodiwa hapa nchini kati ya mwezi Agosti na Septemba mwaka 2021.

Barbara Gonzalez: Tutachukua tahadhari kubwa Afrika Kusini
Mitihani ya Taifa kusahihishwa kidijitali