Waziri wa Viwanda na Biashara Prof. Kitila Mkumbo ametoa wito kwa wafanyabiashara na wawekezaji wenye nia kutoka Uturuki na nchi nyingine kuja kuwekeza na kufanya biashara kwa ubia na Tanzania na Afrika kwa ujumla ili kupata uwiano wa maendeleo (win win Situation) kwa pande zote mbili kupitia Mkataba wa Eneo Huru la Biashara la Afrika (African Continental Free Trade Area-AfCFTA).

Prof. Mkumbo ameyasema hayo alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu Mkataba wa AfCFTA na fursa za masoko katika Kongamano la tatu (3) la Uchumi na Biashara kati ya Uturuki na Afrika lililofanyika Istanbul Uturuki ambapo Kongamano hilo linalenga kuimarisha uhusiano kati ya Uturuki na Afrika katika kuendeleza bishara, uwekezaji na uchumi.

Profesa Mkumbo ameambatana na Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar Omar Shaaban pamoja na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Mazingira David Makiposa, Kaimu Balozi wa Tanzania nchini Uturuki Bw. Hassani Mwamweta na wafanyabiashara wa Tanzania kuhudhuria Kongamano hilo nchini Uturuki.

Akiwasilisha mada yake Prof. Mkumbo amewasihi wawekezaji kutoka Uturuki kuja kuwekeza Tanzania na Afrika kwa ujumla kwa kuwa Mkataba AFCFTA unawezesha upatikanaji wa soko la bidhaa na huduma lenye idadi ya watu takriban bilioni 1.2 ambapo hadi sasa nchi 44 za Afrika zimeridhia Mkataba huo ulioanza kutekelezwa tangu Mei 30, 2020.

Amesema mpaka sasa Mataifa ya Afrika yamepata uhuru wa Kisiasa sasa yaongeze nguvu katika kujikomboa kiuchumi ili kufikia malengo ya Agenda 2063 ya Afrika yenye lengo la kuhakikisha kuwa Afrika inakomesha maisha ya bunduki ndani ya Afrika, kukuza Uchumi, kutunza Amani, kuendeleza Elimu na Sekta ya Viwanda na teknolojia kwa kutumia mkataba wa AfCFTA.

Naye Waziri wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda wa Zanzibar Omar Shaaban alipokuwa akiwasilisha mada kuhusu fursa za uwekezaji katika Kongamano hilo, aliwakaribisha wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania na Zanzibar yenye idadi ya watu takriban milioni 60 ambayo inatoa fursa nyingi za uwekezaji, mazingira bora ya kufanya Biashara, maliasili, vivutio vya utalii, malighafi za kutosha, Uchumi wa bahari na soko la uhakika

Mama aliyetupa mtoto chooni mikononi mwa Polisi
Maajabu ya juisi ya Ubuyu