Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amewataka wakazi wa jiji la Dar es salaam kufuta video na picha za ngono zote walizonazo kwenye simu zao, ili kujiepusha kukumbana na rungu la TCRA.

Ameyasema jijini Dar es salaam alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema kuwa ipo siku TCRA watafanya ukaguzi kugundua nani anahusika na kuvujisha video za ngono mitandaoni, na itakuwa aibu iwapo mtu mzima au kiongozi wa serikali kukutwa nazo.

“Naomba kabla ya Jumatatu wewe Mwana Dar es salaam uliyeweka picha za ngono kwenye simu yako, naomba zifute, TCRA wana uwezo mkubwa wa kufuatilia, heri wafuatilie wakute zilikuwepo lakini zimefutwa, na vile vile unaweza ukajisahau ukaacha simu bila kuweka password mtoto akachukua simu kucheza game, akakutana na picha za ngono, ni aibu,” amesema Makonda.

Hata hivyo, Makonda ameitisha mkutano na waandishi wa habari kuzungumzia mkakati wake wa kukomesha ushoga na biashara ya ngono jijini Dar es salaam ambapo ametangaza kuunda kamati ya kufuatilia vitendo hivyo, ambayo amevitaja kulipa laana taifa.

Tajiri wa PSG kushughulikia usajili wa Paul Pogba
Real Madrid waombwa kusahau yaliyopita