Mwaka mmoja baada ya kushiriki kwenye ngoma ya DJ Khaled, ‘I Got the Keys’, Jay Z na Future wameingia kwenye vichwa vya habari wakidaiwa kukwaruzana kwenye michano.

Jigga ameibua joto la mkwaruzo huo kufuatia maandishi ya ngoma yake kwenye albam yake mpya ya 4:44, kwenye moja kati ya nyimbo za utambulisho aliyoibatiza ‘Kill Jay Z’.

Hov anarap, “I don’t even know what you would’ve done. In the future, other ni**as playin’ football with your son / You would’ve lost it.”

Mistari hiyo imehusishwa na tukio la mtoto wa kiume wa Future aliyezaa na mwimbaji Ciara, kuonekana mara kwa mara akicheza mpira na mume wa mwimbaji huyo ambaye ni nyota wa mpira wa kikapu, Russell Wilson.

Future anadaiwa kumjibu Jigga kwenye snapchat Jumatatu hii, akitumia lugha ya picha na maneno, kwa kupost picha anayoonekana ameweka kitita cha fedha kwenye sikio lake kama simu na kuandika, “U ain’t got the juice like dat. MOOD.”

Hata hivyo, wachambuzi wa tambo na majigambo ya hip hop wameelezea picha na maneno hayo kuwa ametoa jibu kwa Hov kwa kutohoa mistari ya wimbo wa nguli huyo wa rap kwenye wimbo ‘The Story of O.J’ kwenye albam ya 4:44.

 “Y’all on the ‘Gram holdin’ money to your ear / There’s a disconnect, we don’t call that money over here,” Hov anarap.

Mfululizo wa uwepo wa mkwaruzano wa mistari kati ya wakali hao wa michano umekuja ikiwa ni siku chache baada ya Jay Z kumtaja Future kwenye orodha ya watu ambao wamemhamasisha kufikia albam yake ya 4:44.

?LIVE: Yanayojiri Bungeni Dodoma leo Julai 5, 2017
Video: Acacia yatafuta suluhu Marekani, Wapiga dili wamzuia JPM kwenda nje