Fuvu la binadamu anayeaminika kuwa ni mwanamke, limekutwa katika nyumba ya mtu mmoja aliyekuwa akiaminika kuwa mchungaji katika eneo la Akutu, jimbo la Ogun nchini Nigeria.

Huyu huenda angepaswa kujiita ’mchungaji mauzauza’ na sio mchungaji anayewapaka tope wachungaji watumishi wa Mungu waaminifu .

Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Thesunonline kuwa, fuvu hilo lilikutwa ndani ya nyumba aliyopanga mchungaji huyo baada ya mwenye nyumba wake kuingia akiwa na watu kadhaa kwa lengo la kumfukuza kutokana na kutolipa kodi kwa kipindi cha mwaka mmoja.

pichaa

Picha ya nyumba na fuvu lililokutwa

“Yule mchungaji hakulipia kodi kwa mwaka mzima. Mwenye nyumba aliyekuwa amekasirika aliwachukua watu kadhaa kwa lengo la kutaka kumuondoa, lakini walipoingia ndani ghafla walishtuka baada ya kubaini kulikuwa na fuvu la binadamu,” chanzo kiliuambia mtandao huo.

Majirani walivutwa na tukio hilo, umati mkubwa ulijaa katika nyumba hiyo na polisi walifika katika eneo hilo na kumtia nguvuni.

Kulikuwa na ripoti kuwa mchungaji huyo alikuwa ameshatoa ufunuo kanisani kwake kuhusu uwepo wa fuvu hilo nyumbani kwake. Anadaiwa kusema kuwa ni la dada yake. Kwamujibu wake, mama yake alikuwa na watoto watatu, yeye na dada zake wawili ambao alikuwa akiishi nao ndani ya nyumba yake lakini hawakuwahi kuonekana.

Dongo la Rais Buhari kwa mkewe mbele ya Chancellor wa Ujerumani ‘lafufua makaburi’
Unyama: mwanamke amuua mjamzito kwa kumpasua tumbo kwa kisu na kuiba mtoto