Timu za taifa za Msumbiji na Zambia zimepata ushindi katika michezio yao ya mkondo wa kwanza ya kusaka tiketi ya kufuzu fainali za kombe la Dunia ambazo zitafanyika nchini Urusi mwaka 2018.

Msumbiji wamepata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Gaboni, katika mchezo uliochezwa Jijini Maputo, ambapo bao hilo pekee limefungwa na mshambuliaji Helder Pelembe.

Gabon wenyeji wa michuano ya mataifa ya Afrika ya mwaka 2017 walicheza mchezo huo bila ya nyota wao Pierre-Emerick Aubameyang, kutokana na majeraha yanayomkabili.

Mchezo wa marudiano wa timu hizo mbili utafanyika siku ya Jumamosi katika mji wa Libreville huko nchini Gabon.

Zambia wakiwa ugenini katika dimba la Karima nchini Sudan, wakipambana na wenyehi wao timu ya taifa ya Sudan ambao wamekubali kibano cha bao moja kwa sifuri .

Mshambuliaji Winston Kalengo ndiye aliyeipa ushindi Chipolopolo kwenye mchezo huo, kutipia juhudu alizolionyesha katika dakika ya 28.

Zambia watakua wenyeji wa Sudan katika mchezo wa mkondo wa pili utakaofanyika mjini Ndola siku ya jumapili.

Lamine Diack Ajiweka Pembeni Kwa Kashfa
Mbinu za Ukawa Kumtumia Lowassa Uspika Zanaswa