Hatimae klabu ya Man City imekamilisha mpango wa usajili wa kinda kutoka nchini Brazil na klabu ya Palmeiras Gabriel Fernando de Jesus.

Man City wamethibitisha mpango wa kumnasa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19, kupitia tovuti yao ambayo imeeleza kuwa, Jesus atakuwa sehemu ya kikosi kitakachopambana na Tottenham mwishoni mwa juma hili.

Mshambuliaji huyo alikubali kujiunga na Man city mwanzoni mwa msimu huu, lakini aliendelea kubaki nchini Brazil, kutokana na baadhi ya mambo ya uhamisho wake kukwama.

Jesus anakua mchezaji wa sita kusajiliwa na meneja wa sasa wa Man City Pep Guardiola, tangu alipowasili klabuni hapo mwanzoni mwa msimu huu akitokea FC Bayern Munich.

Jesus, ana uwezo wa kucheza nafasi yoyote ya ushambuliaji, hali ambayo inaaminiwa na meneja huyo kutoka nchini Hispania huenda ikamsaidia katika harakati za kutibu majeraha ya kupoteza muelekeo katika ushindani wa ligi ya nchini England.

Mutungi akata mzizi wa fitina CUF,asema yeye hajaandika katiba ya chama hicho
Wenye Diploma waula,sasa kuanza kupata mikopo