Mshambuliaji kutoka nchini Brazil Gabriel Jesus, ametegua Kitendawili cha ushangiliaji wake kila anapofunga bao, baada ya kushindwa kufanya hivyo kwa miaka kadhaa.

Jesus ametegua Kitendawili hicho, saa chache baada ya kukamilisha taratibu za kujiunga na klabu ya Arsenal inayoshiriki Ligi Kuu ya England, akitokea kwa Mabingwa wa nchi hiyo Manchester City.

Mshambuliaji huyo amesema aina ya ushangiliaji wake ambao huonyesha ishara ya kupiga siku, ina maana kubwa, kwani inahusisha Maisha aliyowahi kupitia tangu akiwa mtaani anaosha magari.

Amesema dharau inayotokana na kutokua na kitu, na watu kukujali baada ya kuwa na kitu, imekua chagizo kubwa la kukumbuka kitendo hicho ambacho aliwahi kufanyiwa na msichana aliyetokea kumpenda.

“Nilimpenda msichana sana, kila wakati nilimpigia simu hakupokea simu zangu, kwa sababu nilikuwa muosha na msafisha magari. Nilipokuwa naanza kucheza ligi kuu (Premier league) na timu ya taifa ya Brazil nilikuwa tajiri Sana, yeye ndiye alikuwa wa kwanza kumpigia lakini sikuwahi kupokea simu yake kila nilipofunga goli nashangilia kwa ishara ya kuongea na simu kumkumbusha ya zamani.” amesema Jesus

Jesus anatarajiwa kutambulishwa kwa Mashabiki wa Klabu ya Arsenal wakati wowote kuanzia sasa, huku akipewa nafasi kubwa ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza cha Mikel Arteta msimu ujao wa 2022/23.

Mgogoro wa mpaka wazusha mapigano
Polisi wajeruhiwa wakiwatawanya waandamanaji