Mlinzi wa pembeni wa vinara wa msimamo wa ligi kuu Tanzania Bara (VPL) Simba SC Gadiel Michael Mbaga, amesema hajapoteza mwelekeo ndani ya kikosi cha mabingwa hao, kufuatia kukosa namba ya kudumu  kutokana na kuwekwa benchi mara kwa mara na Mohammed Hussein “Tshabalala”.

Gadiel amesema dhana ya mashabiki kuwa mchezaji akitoka Young Africans kwenda Simba SC hawawezi kuonyesha kiwango kizuri sio sahihi, kwani inategemea na mchezaji mwenyewe kujitambua na kujua anataka nini katika soka.

Beki huyo ambaye pia aliwahi kuitumiki Azam FC kabla ya kutimkia Young Africans amesema, anapenda sana ushindani kama alivyoukuta Simba SC, hivyo hana shaka kwa kuamini hali hiyo inaendelea kumjenga na kuimarisha uwezo wake mazoezini ili kumshawili kocha.

Amesema kabla hajasaini Simba SC tayari alikuwa anajua ubora wa Mohammed Hussein kwakua alikua anamuona walipokua wakicheza kwenye kikosi cha timu ya taifa (Taifa Stars) na yeye akawa anaanza huku Tshabalala akisubiri Benchi.

Ronaldo amtimulia vumbi Messi
Watuhumiwa wamekiri kufanya mauaji ya dereva taksi (uber)