Mshambuliaji kutoka nchini Italia, Super Mario Barwuah Balotelli huenda akarejeshwa kwenye klabu yake ya Liverpool mwishoni mwa msimu huu, kufuatia kushindwa kufikia lengo la kuushawishi uongozi wa klabu ya AC Milan ambao ulimsajili kwa mkopo mwanzoni mwa msimu huu.

Mtendaji mkuu wa klabu ya AC Milan, Adriano Galliani amethibitisha kuwepo kwa uwezekano wa mshambuliaji huyo kurejeshwa nchini England, kutokana na kiwango chake kutowaridhisha mpaka sasa.

Galliani amesema ni vigumu kwa sasa kuamini kama wataendelea kuwa na Balotelli, ambaye walidhamiria kumsajili moja kwa moja mwishoni mwa msimu huu, kutokana na kiwango chake duni alichokionyesha.

Amesema mpaka sasa Balotelli, amefanikiwa kufunga mabao matatu katika michezo 17 aliyocheza, hali aambayo inawakatisha tamaa wao kama viongozi ambao wamekua wakipokea taarifa kutoka kwenye benchi la ufundi.

‘Tunampenda sana Mario, lakini ameshindwa kutushawishi katika harakati za kuendelea kubakia hapa, kutokana na makubaliano tulioingia na uongozi wa Liverpool ya kumsajili moja kwa moja kama tutaridhika na uwezo wake.’ Amesema Galliani

‘Mario amekua na mazingira mazuri tangu alipojiunga nasi, lakini tunashindwa kufahamu kwa nini anafikia hatua ya kurejea katika kiwango chake kama ilivyokua siku za nyuma akiwa na klabu za Inter Milan, Man City, Liverpool na hata tulipomsajili akitokea Man City mwaka 2013.’ Aliongeza kiongozi huyo

Balotelli, mwenye umri wa miaka 25, alikua na uwezo mkubwa wa kusakata kabumbu katika msimu wa 2013-14 aliposajiliwa na AC Milan akitokea Man City ambapo alicheza michezo 54 na kufunga mabao 30.

Antonio Conte Amtolea Macho Winga Wa Inter Milan
Video: TAKUKURU Waingiza Miguu Yote Sakata La upangaji Matokeo