Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amelitaka Baraza Kuu la Waislamu mkoani Arusha kukemea tabia ya baadhi ya waumini wa dini ya kiislam kucheza mchezo wa kareti misikitini na kusisitiza kwamba tabia hizo haifai

Ameyasema hayo mkoani Arusha mara baada ya kumalizika kwa ibada ya sikukuu ya Eid iliyofanyika katika uwanja wa Sheikh Amri na kuwataka Bakwata kukemea tabia hiyo.

Amesema kuwa tabia ya baadhi ya misikiti kufundisha waumini wake mchezo wa kareti ndani ya misikiti haifai na inapaswa kukemewa.

“Baadhi ya misikiti kufundisha karate haifai naomba niwapongeze Bakwata kwa kukemea tabia hii na ninawaomba muendelee kulisimamia hili,”amesema Gambo

Mmiliki wa shule Jijini Dar ajimiminia risasi hadi kufa
Habari kubwa katika Magazeti ya Tanzania leo Juni 16, 2018