Mkuu wa mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo jana Disemba 10,2017 ameweka picha kwenye mtandao wake wa Facebook akiwa na Mbunge wa Arusha Mjini kwa tiketi ya CHADEMA,  Godbless Lema huku akisema kuwa yupo mbioni kurudi nyumbani.

Aidha, baada ya kuweka picha na ujumbe huo baadhi ya watu walianza kusema kuwa Mkuu wa mkoa huyo anafanya siasa rahisi huku wengine wakisema ni jambo ambalo haliwezekani Mbunge huyo wa CHADEMA kurudi CCM.

Hata hivyo, ujumbe huo ulizua mjadala mkubwa katika mitandao ya kijamii kuhusu mbunge huyo kurudi ndani ya chama cha mapinduzi.

 

Netanyahu: Jerusalem ni mji mkuu wa Israel
Japan, Marekani na Korea ya Kusini kusaka njia za kujihami