Serikali Mkoani Arusha imesema busara ilipaswa kutumika zaidi katika Utekelezaji wa Agizo la Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alilotoa wakati wa ziara yake Wilayani Karatu katika Bonde la Eyasi kuhusu kusogezwa kwa Mashine za kuvuta maji umbali wa Mita 500 kutoka chanzo cha Maji.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo, alipokuwa katika ziara yake ya kikazi Wilayani Karatu, amesema kutokana na umuhimu wa bonde la Eyasi katika uzalishaji wa Chakula haikuwa busara kwa wananchi kuchoma mashine hizo bila kujali mazao ambayo tayari yamesha oteshwa katika eneo hilo na gharama zilizotumika kununua mashine hizo.

“Vyombo vya ulinzi na usalama vipo kwanini wananchi hawa wasiende kuripoti tatizo hilo kwenye vyombo vinavyohusika na badala yake wanaamua kujichukulia sheria mikononi, Kisheria hairuhusiwi kwa mtu yeyeote kuharibu mali ya mwananchi, ilikua ni lazima tuwachukulie hatua wote waliofaya uharibifu huu,” amesema Gambo.

Gambo ameongeza kuwa haikuwa rahisi kwa wananchi wa Mang’ola kuamua kufanya zoezi lile peke yao inaonekana kuna viongozi wa kisiasa ambao wako nyuma ya vurugu zile na sisi kama Serikali tunaamini jukumu la kiongozi ni kuleta amani na sio uvunjifu wa amani na ukienda kinyume sheria inafuata mkondo wake.

 

#HapoKale
Jerry Muro Arusha Dongo Msimbazi