Katika kuhakikisha anamaliza tatizo la migogoro ya ardhi Jijini Arusha, Mkuu wa mkoa huo Mrisho Gambo, ameongoza vikao mbalimbali vya kutafuta suluhu ya mgogoro wa Pori Tengefu ambao umechukua muda mrefu.

Aidha katika ziara ya Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, mwezi desemba mwaka jana alimwagiza Mkuu wa mkoa kuwakutanisha wadau wote na kupata maoni yao ili kumaliza mgogoro huo.                                                              

 Wajumbe wamekutana na kujadili chanzo na hatua zilizochukuliwa pia wametembelea eneo lilikusudiwa kutengwa kwaajili ya mapito ya wanyama na mazalia ya nyumbu sanjari na kuangalia vyanzo vya maji na miundombinu.

Gambo amesema serikali iko makini kuangalia njia bora za uhifadhi huku wananchi wakiendelea na maisha yao ya ufugaji bila kuathiri sekta ya utalii kwa ujumla huku maslahi ya wawekezaji yakilindwa kwani wana mchango mkubwa katika kusukuma mbele maendeleo ya taifa yanayotokana na kodi wanazolipa.

Hata hivyo,Taasisi mbalimbali zimeshiriki katika vikao hivyo zikiwemo TANAPA, NCAA,  Tawiri, Asasi za kiraia, Jamii ya wananchi wanaoishi Loliondo na Serikali ya Mkoa na Wilaya.

#HapoKale
Walia na Bodi ya mikopo kuwakata 15%