Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewataka wanaume waliopo katika mahusiano na wanawake ambao hawana mawazo ya kupambana na hali ya uchumi ilivyo kwasasa kujiondoa katika mahusiano hayo kwani ni hatari kwa maisha ya baadaye.

Amesema kuwa mwanaume kama anataka kuwa na uchumi imara kwa sasa hivi ni bora akaachana na mwanamke ambaye anapenda starehe na kuwa na mwanamke mwenye kutoa ushauri mzuri namna ya kupambana na maisha.

“Mwanaume kama una nia ya dhati ya kuwa na uchumi imara kwa kipindi hiki cha uchumi mgumu, basi unatakiwa uepukane na wale wanawake wa aina ya bebi nina njaa, ni bebee pizza au chipsi kuku, usisahau kuweka mayonaise, au bebe simu Iphone X imetoka naomba uninunulie, huo ni Ujuha.”amesema Gambo

Hata hivyo, Gambo amesema kuwa mwanamke mzuri ni yule anayeweka kipaumbele cha maendeleo na kushauriana namna gani ya kuweza kupiga hatua katika maisha.

Polisi ahukumiwa kifungo cha maisha jela kwa kuwapiga risasi waandamanaji
Video: Bao la mkono lamshtua Fatma Karume, sasa akimbilia mahakamani