Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amesema kuwa kama wapinzani wasipobadili mfumo wao wa siasa watapotea kwani Serikali ya awamu ya Tano haina imedhamilia kuwatumikia wananchi.

Amesema kuwa kama wapinzani wataendelea na siasa za porojo na zisizo na msingi watapotea hivyo amewaasa kumuunga mkono rais Magufuli katika kutekeleza ahadi aliyowaahidi Watanzania.

“Nataka niwaambie wanasiasa hawa wa upinzani wasipobadilisha aina ya siasa wanayofanya kwa ninavyoona mimi Serikali ya awamu ya tano watapotea, kwa sababu tumepata Rais ambaye hatanii, unajua wameshazoea wengine wakitishwa tishwa kidogo wanaingia mitini huyu Magufuli akinyooka amenyooka, ananyoosha rula tu utaamua mwenyewe ukae kushoto au kulia. Kwa hiyo mimi niwashauri tu itakuwa vizuri badala ya kupiga porojo wajipange kumsaidia Rais aweze kutekeleza mambo aliyoahidi kwa Watanzania kwa miaka mitano,”amesema Gambo

Hata hivyo, Gambo ameongeza kuwa mtu yeyote atakayejaribu kukwamisha Serikali ya awamu ya Tano isitekeleze malengo yake basi watakula naye sahani moja.

 

Liverpool kumng'oa Chamberlain Arsenal
Pacquiao adai hataangalia pambano la Mayweather Vs McGregor kwa sababu hizi