Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo amewataka viongozi wa CHADEMA jijini humo akiwepo Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema pamoja na Meya wa Jiji la hilo, Calist Lazaro kushirikiana na serikali.

Gambo ameyasema hayo baada ya viongozi hao wa CHADEMA ambao anadai walikuwa wamealikwa kushiriki katika zoezi la utoaji wa mikopo kwa kina mama kutotokea kwa kuwa zoezi hilo lililokuwa likisimamiwa na serikali.

“Nipende kutumia fursa hii kuwaomba viongozi wenzangu bila kujali itikadi ya vyama vyao maana leo tulimualika hapa mbunge, Meya na madiwani lakini wakasema tu sisi hatuendi sababu lile jambo linasimamiwa na serikali, mimi nataka tu niwaombe viongozi wenzangu kwamba masuala ya maendeleo hayana vyama kwa sababu na sisi pia tungeangalia vyama pengine tungewaambia watu wa CCM wawape tu mikopo hiyo wanachama wao lakini tukasema sisi wenye serikali watu wetu ni wote bila kujali itikadi ya vyama vyao hivyo niwaombe wakubali kwamba Rais wa Tanzania ni Dkt. John Pombe Magufuli,”amesema Gambo 

Aidha, Gambo amezungumzia suala la maandamano ya April 26, 2018 kwa kusema kuwa wapo watu wanafanya kazi ya kushawishi watu kuandamana lakini wao kama viongozi wanatoa njia za watu kupambana na maisha.

Hata hivyo, ameongeza kuwa kuna watu ambao wanahamisisha maandamano lakini lakini Serikali inatoa mitaji na mbinu mbalimbali na mitaji kwa wananchi ili waweze kujikwamua kiuchumi.

Nondo aachiwa kwa dhamana
Boko Haram wawaonya wasichana waliowaachia kutorudi shule