Meneja wa mpya wa klabu ya Aston Villa, Remi Garde amepasua ukweli wa jambo lililomsukuma kukubali kufanya kazi na uongozi wa klabu hiyo inyoshiriki ligi kuu ya soka nchini England.

Garde, alitangazwa kuchukua nafasi ya kuajiriwa klabni hapo siku mbili zilizopita, kufuatia kutimuliwa kwa Tim Sherwood majuma mawili yaliyopita, kutokana na matokeo mabovu yaliyokua yamekithiri huko Villa Park.

Garde, amesema ilikua ni vigumu kwake kukubali kujiunga na klabu ya Aston Villa, kutokana na kufahamu ugumu wa mazingira ya kazi klabuni hapo, lakini ushauri alioupata kutoka kwa aliyewahi kuwa meneja wa The Villians, Gerard Houllier, ulimpa ujasiri na kuafiki ombi lililowasilishwa kwake.

Amesema ukaribu uliopo kati yake na Gerard Houllier, ulikua chagizo la kuafiki suala la kuajiriwa klabuni hapo kutokana na maneno mazuri aliyomuambia na anaamini yatamsaidia katika utendaji wake wa kazi zake za kila siku.

Amesema meneja huyo ambaye pia aliwahi kukinoa kikosi cha Liverpool, amemuhakikishia hakuna jambo ambalo litaweza kumshinda katika utendaji wake wa kazi, kutokana na kumfahamu vizuri, hivyo amesisitiza kuwa tayari kuwajibika ipasavyo na kufikia lengo linalokusudiwa.

Garde, aliwahi kufanya kazi na Gerard Houllier, walipokua kwenye klabu ya Olympic Lyon ya nchini Ufaransa kuanzia mwaka 2005–2007 na walifanikisha baadhi ya mambo katika utendaji wao wa kazi, kabla ya babu huyo kuamua kurejea nchini England mwaka 2010.

Baada ya kuondoka kwa Gerard Houllier, Remi Garde, alikabidhiwa kikosi cha Olympic Lyon ambapo alifanya kazi hiyo hadi mwaka 2014 na sasa ameelekea nchini England kujiunga na na klabu ya Aston Villa inayohitaji msaada wa kusaka mafanikio ya kujikwamua na matokeo mabovu.

Garde atakabiliwa na matihani wake wa kwanza katika ligi ya nchini England, mwishoni mwa juma hili, ambapo kikosi chake cha Aston Villa kitapambana na vinara wa ligi ya nchini England Manchester City.

Amir Khan Apewa Ushauri Wa Bure
Picha Za Ngono Zampeleka Pabaya Benzema